Thursday, September 29, 2011

MMhhh!!!!!!!!!!Mcharuko........


                                                        Rose akifanya vitu vyake
Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Rose, hivi karibuni alinaswa akicheza muziki kihasarahasara kiasi cha kuwafanya baadhi ya wadau kumpachika jina la Jimama Mcharuko,

Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilijiri ndani ya Ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilipokuwa inaporomosha burudani pande hizo.

Awali, mama huyo alitinga maeneo hayo akiwa ndani ya gari lake aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T 108 AWP na moja kwa moja alikwenda kwenye meza kuu ya kuuzia vinywaji ‘kaunta’.

KINYWAJI KINAKOLEA
Baada ya mwanamke huyo kuketi, aliagiza kinywaji na kuanza kukigida kwa staili ya aina yake hadi akawa tilalila ambapo baadaye alijitupa kwenye ‘dancing floor’ na kulirudi sebene huku akianika baadhi ya sehemu zake nyeti.



Stali yake hiyo ya uchezaji iliwafanya baadhi ya wanaume waliokuwa ukumbini hapo kumkodolea macho huku wengine wakitokwa na udenda kutokana na jinsi alivyokuwa akijianika.

AWATUZA WASANII KWA FUJO
Kama hiyo haitoshi, Rose alipanda jukwaani kwa mbwembwe na kuwatuza wanamuziki huku akijigamba kuwa yeye ni pedeshee wa kike na kuhusu kucheza sebene hakuna anayeweza kumshinda.


Aidha, kila aliyekuwa akimtuza alimkatia mauno na wakati mwingine kujiangusha chini kisha kujigalagaza kama aliyepandwa na mzuka kupita maelezo.
Kufuatia mambo aliyokuwa akifanya mama huyo ukumbini hapo, paparazi wetu alimfuata kwa lengo la kumhoji sababu ya yeye kucheza kihasara kiasi kile ambapo kutokana na jinsi alivyokuwa ‘bwii’, zoezi hilo lilishindikana


ANASWA AKIWA FRESH
Kama Waswahili wasemavyo, milima haikutani ila binadamu hukutana, juzikati paparazi wetu alikutana na Rose ndani ya Ukumbi wa Meeda ulipo Sinza Mori, Dar es Salaam akiwa kwenye mishemishe zake.

Alipobanwa sababu ya siku ile kucheza kihasara kiasi cha kuanika nyeti zake wakati anaonekana ni mke wa mtu alisema: “Nilikuwa na furaha sana, yaani we acha tu, kwa sasa sina kizuizi cha kujirusha kwani mchumba wangu ameshanivisha pete na yuko nje ya nchi, hana mpango wa kurudi leo wala kesho.”

Chanzo na Global pub.

No comments:

Post a Comment