Monday, September 5, 2011

Bongo usiku sooo!!!!!!


Katika kuhitimisha shamrashamra za Sikukuu ya Idd El Fitr, mwishoni mwa wiki iliyopita,kulikuwa na matukio kadhaa ya kutisha jijini Dar nyakati za usiku.


Katika tukio la awali, shabiki mkubwa wa burudani Bongo, Mwajuma Thabit ‘Rose Jimama’ alinaswa akibanjuka kihasarahasara ukumbini na kuwaacha watu midomo wazi.

Rose Jimama alifanya mambo hayo ya aibu kwenye onesho la Bendi ya Stone Mayiyasika ndani ya Ukumbi wa Green Park, Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuvamia jukwaa baada ya kudatishwa na sebene la bendi hiyo, alikwenda mbele zaidi na kugeuka kero alipokuwa akiwafuata wanaume waliotimba na wake zao kisha kuwakatia mauno jambo lililowakera watu.

Katika tukio lingine, nao watoto wa kishua ‘vigogo’ walinaswa wakijiachia kihasarahasara katika Ufukwe wa Mbalamwezi Beach, Dar usiku wa Ijumaa iliyopita ambapo kulikuwa na tamasha lililokwenda kwa jina la Miami Beach Part lililokusanya idadi kubwa ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.

Wakiwa katika shangwe za hapa na pale, watoto hao wa ‘wakubwa’ walionekana wakijiachia na vinguo vifupi vilivyoacha nje maungo yao nyeti bila kujali uwepo wa watu wa kada mbalimbali.

No comments:

Post a Comment