Thursday, September 29, 2011

Isha: Akha! Sina matiti...




MWIMBAJI na mtunzi mahiri wa Kundi la Taarab la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan ‘Mashauzi’ (pichani), ameshtuka na kusema katu ukubwa wa matiti yake hautokani na madawa ya kukuza viungo yanayotoka China.
Mashauzi aliyasema hayo Alhamisi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar katika moja ya shoo zake.

Akiwa amevalia nadhifu stejini, siku hiyo, Mashauzi alionekana kukonga nyoyo za mashabiki wake hususan alipoimba kibao cha Mama Nipe Radhi.

Baada ya kumaliza wimbo huo na kushuka, ndipo paparazi mmoja alimfuata na kumbana akitaka kujua siri ya ukubwa wa matiti yake kwa sababu kuna watu wanamtuhumu kutumia dawa za Kichina.

Akafunguka: “Kimsingi wengi hufikiri hivyo, lakini msema ukweli ni mpenzi wa Mungu, haya ni matiti yangu ya kuzaliwa, ila kuna wanawake wanavutiwa na ukubwa wake.
“Sikatai kwamba wapo wenzangu na miye wanaotumia Mchina kukuza matiti, wengine hata makalio lengo waweze kuwa na soko hapa mjini, mimi sina muda huo na siwezi kumkosoa Mola kwa uumbaji wake,” alisema Mashauzi.


picha kwa hisani ya global

No comments:

Post a Comment