Thursday, September 29, 2011

Askari Polisi Aliyeuwawa Kwa Kupigwa Nondo MkoanI Mbeya Aagwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evance Balama akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa askari Polisi PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi akitoa heshma za mwisho kwa mwili wa askari Polisi PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi
Askari Polisi wakitoa wakitoa heshma za mwisho kwa mwili wa askari mwenzao, PC Meshack Urasa ambaye aliuawa kwa kupigwa na nondo juzi Jijini Mbeya. Mwili wa marehemu ulisafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Maafisa wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoani Mbeya wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa askari Marehemu Meshack Urassa, upande wa kulia ni Kamanda wa uhamiaji wa mkoa wa Mbeya, akifuatiwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi, anayefuata Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama, anayefuata Kamanda wa Jeshi la magereza mkoani Mbeya na wengineo.
Mke wa marehemu Urassa akishindwa kujizuia baada ya kuuaga mwili wa marehemu mumewe.

Picha kwa hisani ya Global pub.


No comments:

Post a Comment