Monday, September 5, 2011

WOLPER,KABULA WAZINGUANA BAA


 MASTAA wanaotamba katika tasnia ya filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’na Jacqueline Wolper, juzikati walitifuana katika mzozo ulioibuka kati yao baada ya kupombeka ile kinoma.

Filamu hiyo ya bure ilitokea siku ya pili ya Sikukuu ya Eid El Fitr katika ‘pub’ ya staa mwingine wa filamu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ pande za Mwananyamala Kwa makoma jijini Dar baada ya Jini Kabula kuzidiwa na ulabu.

Ghafla alianza kuzozana na Wolper kwa kisa ambacho hakikufahamika na mwenzake alipokuwa akimjibu ndipo alipofikia hatua ya kumvurumishia chupa iliyomkosakosa sehemu za kichwani.

“Ilikuwa ni bahati tu ya Wolper kwani alikwepa, kama ingempata ingempasua vibaya,” baada tukio hilo, timbwili zito liliibuka kati ya wasanii hao ambapo waliamuliwa na wasamaria wema.

No comments:

Post a Comment