Monday, September 12, 2011

BENKI YA NBC YAKABIDHI MSAADA KWA WAHANGA WA TUKIO LA AJALI YA MELI ZANZIBAR, YAFUNGUA AKAUNTI MAALUMU.


 Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja
(kushoto) akikabidhi sehemu ya misaada iliyotolewa na NBC kwa ajili ya
wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander kwa Waziri wa Afya wa
Zanzibar Juma Haji Duni Mjini Zanzibar


Ofisa Uhusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina (wa pili kushoto)
akisaidiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wakazi wa
Zanzibar kushusha baadhi ya vitu vilivyotolewa msaada na benki hiyo.

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa ajili ya tukio la ajali ya Meli ya abiria iitwayo MV Spice Islander iliyozama katika Bahari ya Hindi Visiwani Zanzibar na kupotea idadi ya watu na kuacha majeruhi wengi.

Akikabidhi misaada hiyo kwa Waziri Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji, Meneja wa Tawi la Benki ya NBC mjini Zanzibar, Rajabu Maalim alisema NBC imepokea taarifa za tukio hilo kwa masikitiko makubwa mno kwani baadhi ya waliopoteza maisha na majeruhi ni wateja wa NBC au ni ndugu na jamaa za wateja wetu au wafanyakazi wa NBC.

“Sisi kama Benki ya Taifa ya Biashara baada ya kupokea taarifa hizi tumeona ni vyema tukajitokeza kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali na taasisi nyingine zisizo za kiserikali ili kujaribu kuokoa maisha ya majeruhi wetu wa ajali hiyo ambayo imeitikisa nchini yetu.

Pamoja na kukabidhiwa kwa misaada hiyo ya madawa, vyakula, nguo , na maji yenye thamani ya shs milioni tano, Benki ya NBC pia imefungua akaunti maalumu katika Tawi la mjini Zanzibar iitwayo MV Spice Maafa Account yenye Namba 021206007793 ili kuwapa fursa wananchi kujitokeza kutoa michango yao ambayo itapelekwa moja kwa moja kwa chombo kinachoratibu tukio la ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment