Monday, September 26, 2011

LULU TENA

Lulu baada ya kutajwa  akisubiri zoezi hilo
Wakijiandaa kabla ya kuanza kudendeka
KATIKA kudhihirisha kuwa amekatika mshipa wa aibu, staa kinda wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kwa mara nyingine anatengeneza kichwa cha habari, safari hii ikiwa ni kudendeka hadharani na mwanaume.

 wakidendeka
Tukio hilo la aibu lililonaswa ndani ya viunga vya Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam, Septemba 18, mwaka huu kwenye ‘bethidei’ ya muigizaji mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

Katika tukio hilo, kulikuwa na utaratibu wa kusoma kuponi yenye maelekezo mbalimbali kwa waalikwa.
Utaratibu ulikuwa hivi; Kama mmoja wa waalikwa alishindwa kufanya kile kilichoandikwa kwenye kuponi, alitakiwa kulipa faini ya shilingi 10,000.


wakiwa wameanguka
Ratiba iliendelea kama ilivyopangwa lakini wengi walishindwa kuamini macho na masikio yao baada ya jina la Lulu kufikiwa kwani ilibidi wale wenye ustaarabu na heshima zao watazame pembeni kukwepa aibu ya msanii huyo.

baada ya kudendeka
akiwa ameshikilia kinywaji

wakiwa katika pozi
LULU ATAKIWA ‘KUDENDEKA’
Kuponi ya Lulu ilimtaka atafute mtu anayempenda kisha ‘amkisi’ bila kujali kama ni mwanaume au mwanamke.
Wakati wengi waliamini Lulu angelipa shilingi 10,000 na kuachana na mpango wa kudendeka, msanii huyo ‘aliwasapraizi’ waalikwa wenzake kwa kumtafuta mwanaume na kula naye denda hadharani.

Awali, baada ya kusoma kuponi hiyo, Lulu kwa kujiamini, aliinua macho huku na kule, kisha akamchagua msanii mwenzake, Soud Ally ‘Akui’ kabla ya kusogea naye mbele na kuanza kudendeka.

Kabla hawajaanza ‘upuuzi’ huo, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Issa Twaha ‘Nteza’ aliwahesabia hadi tatu na kuwaacha wajinafasi.

Bila tone la nishai, Lulu alidendeka ‘laivu’ na jamaa huyo hadi wakadondoka chini ambapo baadhi ya watu walisikika wakisema: “Ama kweli Lulu anakoelekea sasa ni pabaya.”

LULU ACHEKELEA
Baada ya mshikemshike huo, wawili hao waliachiana, wakasimama huku Lulu aliyekuwa amevalia kipensi kifupi kilichoacha nje mapaja akibaki anachekelea.

LULU AMEKUWA SUGU?
Lulu mwenye miaka 18 amesharipotiwa na matukio lukuki ya aina hiyo ikiwemo kulewa tilalila na kufanya vitimbi visivyovumilika katika uso wa jamii.
Picha kwa hisani ya Globalpub.

No comments:

Post a Comment