Miss Universe 2011 kutoka Angola, Leila Lopes.
Mshiriki kutoka Tanzania, Nelly Kamwelu.
MTANZANIA Nelly Kamwelu ameshindwa kufanya vizuri katika shindano la Miss Universe 2011 katika fainali ya mchakato huo uliofanyika juzi Jumanne jijini Sao Paolo nchini Brazil.Katika fainali hizo mshiriki kutoka Angola, Leila Lopes amefanikiwa kutwaa umalkia wa taji hilo, huku akimwaga Vasuki Sunkavalli kutoka India ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo.
Leila mwenye umri wa miaka 25 amewashinda washiriki wengine 88 kutoka mataifa mbalimbali ikiwa ni mara ya 60 kwa mashindani hayo kufanyika. Ushindi wa Leila unamfanya awe Miss Universe mpya akichukua nafasi ya Ximena Navarrete wa Mexico.”Nashukuru Mungu kwa jinsi alivyoniumba, kwa kuwa nisingekuwa na uwezo wa kubadili chochote,” alisema Lopes mara baada ya ushindi huo.
Nelly alitwaa taji la Mis Universe Tanzania mnamo Mei 27, mwaka huu, pia hakufanikiwa kuingia katika kumi bora baada ya nafasi hizo kwenda Australia, Costa Rica, Ufaransa, Ukraine, Ureno, Panama, Philippines, Angola, China na Brazil.
No comments:
Post a Comment