Wednesday, September 7, 2011

MWANAMKE ATEMBEAYE NA KUNDI LAKE LA NGEDERE

Tibbs akiwa na ngedere wake
Connie Tibbs akiwa  na ndegere na familia yake. Kutoka kushoto kwenda kulia ni mumewe, Steve, Dalton, Victoria and Tanner.

MWANAMKE Connie Tibbs, amejikuta katika ulimwengu wa kupenda kutembea na kundi lake la ngedere kila anapokwenda na kila anapokaa na kupumzika.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Marekani, mwanamke huyo ambaye ameolewa na mwenye umri wa miaka 37, mkazi wa Pekin, Jimbo la Illinois, Marekani, anawapenda sana wanyama wake hao kiasi kwamba hawezi kuachana nao hata kidogo.

Upendo wake huo humfanya aingie gharama kubwa ya kuwanunulia chakula ngedere hao watano kila wiki – chakula kikubwa kikiwa ni ndizi!
“Wanyama hawa nao wananipenda ajabu kama wanangu, kiasi ukimvuta mmoja kutoka kwangu ni lazima atapiga kelele,” anasema mama huyo na kuongeza kwamba: “Mimi ni mama yao, ulimwengu wao uko kwangu.”

Tibbs anasema kwamba mumewe, Steve, huparurwa na wanyama hao kila anapotaka kuwasogelea. Siyo hivyo tu, mumewe huyo hulalamika kwamba mkewe huwabusu zaidi na kuwashughulikia wanyama hao kuliko anavyomfanyia vitu hivyo yeye.

Wakati ambapo binti yake mdogo, Dalton (13), na Victoria (12) wamezoea tabia hiyo ya mama yao kuwapenda wanyama hao, Tibbs anasema, mtoto wake wa kiume Tanner (17) hawapendi kabisa wanyama hao ambao wanaitwa Alley, Jackson, Audrey, Dexter na Jaeda.
Tibbs akiwanunulia ngedere wake ndizo kwenye supameketi huko Pekin.

Ngedere akijaribu kuendesha gari.
  Steve Tibbs na Dalton (katikati), na Victoria, wakiwa na ngedere hao wakati wa kuogelea. 
 Ni zamu ya ngedere Alley kulala kitandani na binadamu.
 

No comments:

Post a Comment