Siku chache baada ya mwanamuziki wa miondoko ya dansi nchini, Aimerichard Mwamba ‘G-Seven’ kumvisha pete ya uchumba, Suzane Chubwa a.k.a Queen Suzy mwanzoni mwa wiki hii amemtolea posa kwa lengo la kumbeba jumla.
Tukio hilo lilifanyika nyumbani kwa Queen Suzy pande za Kinondoni. Baba yake mkubwa aitwaye Emmanuel Mkude ndiye aliyeipokea barua ya posa na kuahidi kuitolea majibu ndani ya wiki moja.
Mashuhuda wa upande wa Queen Suzy ambaye ni mnenguaji wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ walikuwa ni mama yake mkubwa, mjomba’ake aitwaye Ally na dada yake, Joan.
G-7 aliwakilishwa na Nyoshi El-Saadat ambaye ndiye aliyetoa barua ya posa, Mulemule FBI, Pablo Masai, Balle a Terre na Elombe Kinja ambao waliwawakilisha wazazi wake.
Alipoulizwa sababu za shughuli hiyo kufanyika nyumbani kwake badala ya kwao, mnenguaji huyo alisema wazazi wake wameshafariki hivyo hakuona haja ya kutafuta eneo lingine tofauti na hapo.
“Wazazi wangu walishafariki, waliobakia ni baba mkubwa, dada na mjomba ambao wote wanaishi mbalimbali. Niliona tukutane hapa ili iwe rahisi kujumuika wote kwa pamoja,” alisema Queen Suzy.
No comments:
Post a Comment