Tuesday, April 16, 2013

GHANA YA TINGA FAINALI MWAKATUNDU CUP

Ghana Fc
TIMU ya soka ya Ghana Fc imeendelea kuonyesha ubabe katika mchezo wa soka  baada ya kuichapa goli 1-0 timu ya Majengo Fc katika  michuano ya Mwakatundu Cup katika uwanja wa shule ya msingi Mbata jijini hapa.
Mchezo huo ulio kuwa umevuta hisia za mashabiki wengi katika jijini hapa kutokana na timu hizo kila zinzpokutana  huwa kunakuwa na upinzani mkubwa kwani kila timu huwa inakamia  kupata ushindi dhidi ya mwenzake.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyokuwa  imefanikiwa  kumfunga  mwenzake kutokana kila timu kuwa makini na kutoruhusu wapinzani kushambulia ngome yao hali iliyo zua upinzani mkali katika mchezo huo.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ilkuweza kujipatia ushindi ambao utawezesha timu hiyo kutinga fainali,lakini timu ya Ghana ndiyo ilinufaika na mabadiliko hayo kwani ilijipatia goli la mapema katika kipindi chapili.
Baao la peke la Ghana Fc liliwekwa kimiani dakika ya 57 na Brayttoni  Mponzi baada ya kuwazidi ujanja  mabeki  wa Majengo Fc nakuagiza shuti kali lililoenda kukwamisha mpira wavuni moja kwa moja.
Hadi  dakika 90 za mchezo zina malizika Ghana ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli moja lililo wakatia tiketi ya kutinga fainari huku Mjengo wakiachwa na huzuni ya kuzimiwa ndoto yao ya kutinga fainali.


chanzo na Global

No comments:

Post a Comment