Tuesday, August 30, 2011

USILOLIJUA KUHUSU JUISI YA KOPO.

 Bila shaka unapoingia dukani au supermarket kununua juisi ya box, huwa unaamini kuwa iliyoandikwa ‘100% Puer Juice’ huwa ni halisi na ndiyo bora. Kwa kukuongezea imani zaidi, watengenezaji wameweka na neno ‘No Sugar Added’ au ‘No preservatives’ (haikuongezwa sukari wala dawa)!

Kuanzia leo elewa kwamba hayo ni maneno ya kibiashara tu, ukweli hauko hivyo! Umewahi kujiuliza kwa nini maboksi yote ya juisi hiyo yawe na ladha moja tu. Sote tunajua kwamba, kama ni juisi ya machungwa kwa mfano, ukila machungwa matano, yote hayawezi kuwa na ladha moja!

Lakini kwa juisi za maboksi imewezekana kuwa na ladha moja kwa sababu za kikemia zinazofanywa kiwandani wakati wa kuhifadhi juisi hiyo ambayo huweza kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Hivyo siyo kweli kwamba unachokunywa ni asilimia 100 ‘pure’.

No comments:

Post a Comment