Friday, September 9, 2011

WATANO KIZIMBANI KWA MADAWA YA KULEVYA

  Washitakiwa hao kutoka kushoto ni: Ally Haji, raia wa Iran. Wengine ni Watanzania, Aziz Kizingiti, Said Mrisho, Abdulrahman Lugongo na Hamidu Kitwana.
  .Mshitakiwa namba moja, Ally Haji, akitafakari jambo kabla ya kusomewa mashitaka.

Msanii wa filamu, Snura Mushi, akitoka mahakamani hapo na chupa ya chai ambapo amesema alikwenda kwa ajili ya mshitakiwa namba moja, Ally Haji.

WATU watano leo mchana wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na gramu 97,000 za madawa ya kulevya aina ya heroine yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 4.3.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kutokana na uzito wa kesi hiyo kutakiwa kusikilizwa na Mahakama Kuu.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Septemba 23 mwaka huu.


No comments:

Post a Comment