Mashindano yalianza kama hivi.
MADEREVA wa pikipiki zadi ya kumi kutoka katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro jana jioni walichuana vikali katika mashindano ya mbio za pikipiki yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Saba Saba mjini Morogorona kuhudhuriwa na mashabiki kibao.
Mashindano hayo yaliyopamba sikukuu ya Idd el Haj yalikuwa na upinzani mkali ambapo kila dereva alijaribu kuonyesha ufundi wake wa kulichezea pikipiki na kwamba katika mashindano yam bio, Alpha Mtakwa wa kutoka Wilaya ya Morogoro Mjini alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza wakati nafasi ya pili ilishikwa na Hamisi Jangala na Maulid Ahmed kutoka Wilaya ya Kilombero alishika nafasi ya tatu.
Zifuataza ni picha za tukio zima zikionyesha waendesha pikipiki walioanguka, waliogongana, waliokuwa wakiziendesha kwa mbwembwe na matukio mengine ya kuvutia.
No comments:
Post a Comment