Tuesday, April 16, 2013

Airtel na Nokia wazindua Offer Kabambe ya Nokia Lumia 620

Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Batuli Chombo mwandishi wa habari wa Sikuba kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa  Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia  utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju
                            


Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa  simu Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu 
Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Jimy Tara mwandishi wa habari wa ITV kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa  Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia  utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju

* Wateja kupata muda wa maongezi wa dakika 275 bure

* Offa itajumuisha SMS bila kikomo na kifurushi cha internet ya 3.75G cha 3GB

Monday 15 Aprili 2013, Airtel Tanzania imeungana kwa pamoja na kampuni ya Nokia na  kuzindua simu ya Nokia Lumia 620 itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kuunganishwa na huduma ya technologia ya juu kwa
kupitia simu za kisasa na kupata ofa kabambe za bure za muda wa mongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet kwa muda wa mienzi mitatu Nokia Lumia 620 pamoja na simkadi ya Airtel itatoa uwezo tofauti ikiwemo kuunganishwa na internet na mtandao na kuangalia mitandao mbalimbali yakijamii pamoja na tovuti mbalimbali. Nokia Lumia inamuonekano mzuri na wa  kisasa wenye rangi za kipekee ambapo kutokana na ubunifu `wetu wa kutengeneza simu zenye rangi tofauti mteja ataweza
kujichagulia simu yenye mvuto na rangi aitakayo

Vitu vingine vilivyopo kwenye simu hii ya Nokia Lumia ni pamoja na kamera yenye lensi ya kisasa, ya mega pixel 5, pamoja na kamera ya mbele, kutokana na kuwa na Lensi bora hii itamuwezesha mteja kupata video au picha yenye muonekano mzuri zaidi Ndani ya Nokia Lumia 620 unaweza kupata vitu muhimu sana ikiwemo ramani ya Dunia pamoja na maelekezo maalum wa vitu au sehemu maalum mbalimbali, Akiongea wakati wa uzinduzi Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema" tumeshirikiana na Nokia katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora na nafuu kwa kupitia vifaa vya Nokia vinavyokuhakikishia kiwango cha juu huku tukiwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu.

Kwa kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G tunayoitoa nchi nzima wateja wetu wana hakikishiwa huduma za uhakika wakati wote.Nokia Lumia itaunganishwa na ofa ya kifurushi cha muda wa maongezi cha dakika 275, sms bila kikomo na intenet ya kifurushi cha 3GB kitakachopatika kwa wiki moja kila mwenzi kwa muda wa mienzi mitatu "Kupata offa hii wateja wetu watatakiwa kuweka muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi 1000 mara wanaponunua simu ya Nokia Lumia 620. Na katika kuthibitisha thamira yetu ya kutoa huduma zinazoendana nathamani ya pesa ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu.

Airtel itaendelea kushirikiana na makampuni mbalimbali katika kutoa huduma bora na bei nafuu kwa kupitia mtandao wake mpana wenye huduma muhimu za Airtel Money na huduma yetu kabambe ya Airtel yatosha Aliongeza Mmbando.Kwa upande wake Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, alisema kampuni ya Nokia inaendelea kuonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kutoa bidhaa za simu bora zitakazowapatia wateja kile wanachokihitaji.  Tunafurahia kuleta bidhaa bora na za bei nafuu zenye uwezo tofauti, simu ya Nokia Lumia 620katika soko la Tanzania,.Tunaamini  muundo mzuri wa simu hii, rangi nzuri na uzoefu tofauti pamoja na huduma za Airtel zitawapatia wateja wetu sababu ya kujipatia simu hii ya Nokia Lumia"
"Nokia Lumia 620 zinapatikana kwa gharama ya shilingi 450,000/= tu.Simu inapatikana katika maduka yote ya Airtel, midcom na wakala wa Nokia wa premium. kwa sasa, kinachotakiwa kufanya ni wewe mtanzania kutembelea moja kati ya haya maduka na kujipatia simu hii orijino kutoka Nokia.Kutokana na ubora wa simu hizi za Nokia Lumia 620 mteja ataweza kufurahia zaidi huduma zote za kimtandao za Airtel zikiwemo zile za kutuma na kupokea pesa, Airtel Yatosha, Jirushe, kutuma na kupokea
SMS, huduma bora ya Intaneti ya 3.75G na nyingi nyinginezo.




No comments:

Post a Comment