Janet Udegba
Nini tafsiri ya uelekeo wa dunia kutokana na matukio ya kutisha? Upo ukatili mkubwa umefanyika nchini Nigeria ambapo mume amemwagia mkewe mafuta ya petroli na kumchoma moto.Kehinde Adesamuye, 39, mkazi wa Lagos, Nigeria anadaiwa kumchoma kwa moto wa petroli hivi karibuni mkewe Janet Udegba, 35, katika Mtaa wa Ikotun jijini Lagos baada ya kuwa na hasira kutokana na kuhisi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine.
Janet na Mumewe Kehinde Adesamuye
Janet alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa katika eneo lake la biashara akiuza vyakula kabla ya Kehinde kufika hapo usiku huo na kumwagia petroli mgongoni kisha kuwasha moto kwa kutumia kibiriti.Hata hivyo, alisema Wanigeria hawatamwachia huru Kehinde kutokana na kile alichokifanya. Akisimulia mgogoro wao, anasema:
Mume wangu amekuwa na wivu daima. Amekuwa na tabia ya kunipiga kila wakati. Nimejaribu mara nyingi kuachana naye lakini huwa ananitishia kuwa lazima atanidhuru. Niliendelea kuishi naye kwa kuwa nilikuwa na hofu ya maisha yangu, aliwahi kuniambia kuwa sitaweza kutoroka hata siku moja“Serikali lazima ihakikishe kuwa Kehinde analipa kwa kile alichonifanyia. Mimi ni yatima, ninafanya biashara ya vyakula ili niishi. Sasa nimetumia pesa zangu zote kwa ajili ya matibabu. Kwa kweli kwa sasa nahitaji msaada,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.
Kehinde alijaribu kutuma rafiki zake ili wamwombee msamaha kwa Janet lakini alikataa. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.
chanzo na global.
No comments:
Post a Comment