Abiria wakipanda ndege ya Fast Jet, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakielekea Kilimanjaro
Abiria wakiwa ndani ya moja ya ndege za Fast Jet, iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro.
Okite Obakponovwe, raia wa Nigeria, akiwa ndani ya ndege ya Fast Jet, yeye alieleza kwamba huduma za Fast Jet ni bora sawa na zile za Easy Jet ya Uingereza.
Marubani wa Fast Jest, John Lewis (Kushoto) na
Alex Taylor (katikati), wakiwa na mhudumu wa ndege, Jasmine Kaungu, muda mfupi
kabla ya kuanza safari ya kutoka Kilimanjaro kwenda Zanzibar, Aprili 10, mwaka
huu.
Unaweza kutafuta kitu ambacho kinaweza kukufanya usisafiri na Fast Jet kwa sasa lakini ikashindikana. Hii ndiyo kampuni inayotoa huduma bora zaidi na nafuu za usafiri wa anga nchini.
Haina muda mrefu sana tangu ilipojikita kwenye ardhi ya Tanzania lakini ndani ya kipindi hicho kifupi, imeweza kuondoa ile dhana kuwa usafiri wa ndege ni kwa ajili ya watu wenye vipato vya juu.
Aprili 10, mwaka huu, mwanadishi wa makala haya, alisafiri na Fast Jet kati ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar na kuzungumza na abiria 27 na kila mmoja alitoa maoni chanya, kuhusu mapinduzi makubwa yaliyofanywa katika Nyanja ya usafiri wa anga na kampuni hiyo ya ndege.
“Niliwahi kusafiri kwa ndege karibu miaka 17 iliyopita. Baada ya hapo sikuwahi kupanda ndege kabisa kwa maana niliona ni gharama kubwa ambazo sikuweza kuzimudu,” alisema Neyman Ndelijwa, 46, mkazi wa Arusha.
Neyman ambaye alikuwa kwenye ndege akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), akielekea Dar es Salaam, alimweleza mwandishi wa makala haya: “Sasa naweza kupanda ndege, Fast Jet wamerahisha sana maisha ya usafiri.
“Ukiangalia bei ambayo nimelipa, haitofautiani sana na gharama za kawaida za usafiri wa mabasi. Naamini kwamba hivi sasa kila anayesafiri kwa basi, anaweza kupanda ndege na ikawa nafuu zaidi kupitia Fast Jet.”
Anachokizungumza Neyman ni kweli kabisa, kwani mapinduzi ya sasa ya Fast Jet, yanafanya usafiri wa ndege kuwa gharama nafuu mno kupita hata basi.
Mathalan; kwa usafiri wa basi kwenda Mwanza, nauli ni kati ya shilingi 45,000 mpaka 60,000. Fast Jet yenyewe inatoza nauli ya chini kabisa shilingi 43,000, yaani usafiri shilingi 32,000 na kodi shilingi 11,000, jumla shilingi 43,000.
Vilevile unapopanda Fast Jet, haikulazimu kuingia gharama za ziada kwa ajili ya matumizi ya njiani. Kati ya dakika 45 na 60, unakuwa umeshafika unapokwenda.
Unaposafiri na basi, mbali na kutumia saa nyingi njiani, vilevile itakulazimu kununua chakula kuanzia asubuhi, mchana na wakati mwingine jioni, kwani unakuwa bado hujafika. Kwa kifupi, Fast Jet ni mkombozi wa kila Mtanzania.
Hakuna sababu ya kutumia saa nyingi njiani au wakati mwingine kupitisha zaidi ya siku ukisafiri, eti kwa kukimbia gharama za kusafiri kwa ndege, wakati Fast Jet inakusafirisha kwa bei nafuu kuliko hata ile ambayo ungelipa kwa basi.
Musika Nyangabo, 41, aliyekuwa anatokea JNIA kwenda Kia, alisema: “Fast Jet ni nafuu sana. Mimi na mtoto wangu tumeweza kusafiri kwenda na kurudi, Kilimanjaro – Dar kwa shilingi 282,000. Unadhani kama ingekuwa ni kwenye makampuni mengine hali ingekuwaje? Nafurahia bei na huduma za Fast Jet.”
NI HUDUMA KAMA ULAYA
“Ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, Watanzania wana kila sababu ya kujivunia Fast Jet kwa sababu ni kampuni bora sana ya ndege,” alisema Okite Obakponovwe, 37, raia wa Nigeria ambaye alizungumza na mwandishi wa makala haya, akiwa angani kutoka Kia kwenda Julius Nyerere International Airport, Dar es Salaam.
Mnigeria huyo, aliyekuwa Kilimanjaro kwa ajili ya kutalii Mlima Kilimanjaro, aliongeza: “Fast Jet ni sawa na Kampuni ya Easy Jet ya Uingereza. Kila huduma inayotolewa na Fast Jet, inaendana na Easy Jet, kwa kifupi Tanzania imepata bahati kuliko nchi nyingine yeyote Afrika.
Obakponovwe ambaye alikuwa ameongozana na mkewe, Irene Okite, aliongeza: “Gharama ni nafuu sana. Hata kule Uingereza Easy Jet ni nafuu. Mimi na mke wangu, tumefurahia huduma za Fast Jet, tumeweza kusafiri vizuri na ndege zake zina uhakika wa safari na kufika salama kwa asilimia 100.”
Abiria wengine waliozungumza na mwandishi wa makala haya ni Faraja Temu, aliyewasili Uwanja wa Ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume, Zanzibar akitokea Kilimanjaro, yeye alisema: “Nafurahia huduma, Fast Jet imerahisha maisha yetu ya usafiri hata kwetu sisi wanafunzi.”
NDEGE ZA AIRBUS BORA SANA
Mhudumu wa ndege, Jasmine Kaungu, alisema: “Nilishafanya kazi kwenye makampuni tofauti ya ndege hapa nchini, ila najisikia fahari kufanya kazi na Fast Jet. Abiria wanasafiri kwa uhakika sana kutokana na ndege zetu aina ya Airbus ambazo ni bora sana.”
Mmoja wa wasimamizi wa huduma kwa wateja, Omar Chinguile, alisema: “Kikubwa kwetu ni umakini. Menejimenti yetu ipo makini kuhakikisha wateja wanapata huduma bora sana. Ripoti yoyote inayoonesha uzembe, husababisha mfanyakazi apoteze ajira.”
BOOKING YA MAPEMA NI MUHIMU
Mkuu wa Oparesheni wa Fast Jet, Kia, Robert Kessy alisema: “Nashauri abiria wawe wanajitahidi kufanya booking mapema ili wapate bei ya chini kabisa ambayo ni shilingi 43,000. Wanapochelewa ndiyo hukutana na bei za juu. Kwa kawaida bei zetu zinaanzia shilingi 43,000 mpaka shilingi 300,000.”
No comments:
Post a Comment