MANCHESTER United juzi waliendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya England baada ya kuihadhiri Arsenal kwa kuichapa mabao 8-2 kwenye uwanja wa Old Trafford.
Bao la kwanza la Man U lilifungwa na Danny Welbeck katika dakika ya 22 kabla ya Arsenal kukosa penati katika dakika ya 25 na kujikuta wakifungwa bao la pili maridadi na Ashley Young katika dakika ya 28.
Wayne Rooney aliipatia Manchester United bao tatu katika dakika ya 41baada ya kupiga faulo ambayo ilimshinda kipa wa Arsenal, Szczesny na kujaa wavuni, lakini kabla timu hizo hazijaenda mapumziko Arsenal walipata bao ambalo lilifungwa na Theo Walcott aliyepiga shuti katika winga ya kulia na mpira kumpita tobo kipa wa Manchester United, David De Gea katika dakika ya 45.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikitafuta bao, lakini alikuwa Wayne Rooney ambaye alipiga faulo kali katika dakika ya 64 na kutinga wavuni na kuipatia timu yake bao la nne huku kipa wa Arsenal akiwa amesimama.
Katika dakika ya 67 Nani aliipatia Man U bao la tano na katika dakika ya 70 Park Ji-Sung alifunga bao la sita kabla ya Van Persie hajaifungia Arsenal bao la pili katika dakika ya 74.
Rooney aliifungia Man U bao la saba katika dakika ya 81 na Ashley Young alifunga bao la nane na kufunga kitabu hicho cha magoli katika dakika ya 92.
Matokeo ya mechi nyingine yalikuwa Newcastle iliichapa Fulham 2-1, Manchester City iliiadhibu Tottenham 5-1 na Stoke iliichapa West Brom bao 1-0.

No comments:
Post a Comment