Wednesday, April 17, 2013
Tuesday, April 16, 2013
Fast Jet: Hata mtu wa chini kabisa sasa anaweza kupanda ndege
Abiria wakipanda ndege ya Fast Jet, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakielekea Kilimanjaro
Abiria wakiwa ndani ya moja ya ndege za Fast Jet, iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro.
Okite Obakponovwe, raia wa Nigeria, akiwa ndani ya ndege ya Fast Jet, yeye alieleza kwamba huduma za Fast Jet ni bora sawa na zile za Easy Jet ya Uingereza.
Marubani wa Fast Jest, John Lewis (Kushoto) na
Alex Taylor (katikati), wakiwa na mhudumu wa ndege, Jasmine Kaungu, muda mfupi
kabla ya kuanza safari ya kutoka Kilimanjaro kwenda Zanzibar, Aprili 10, mwaka
huu.
Unaweza kutafuta kitu ambacho kinaweza kukufanya usisafiri na Fast Jet kwa sasa lakini ikashindikana. Hii ndiyo kampuni inayotoa huduma bora zaidi na nafuu za usafiri wa anga nchini.
Haina muda mrefu sana tangu ilipojikita kwenye ardhi ya Tanzania lakini ndani ya kipindi hicho kifupi, imeweza kuondoa ile dhana kuwa usafiri wa ndege ni kwa ajili ya watu wenye vipato vya juu.
Aprili 10, mwaka huu, mwanadishi wa makala haya, alisafiri na Fast Jet kati ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar na kuzungumza na abiria 27 na kila mmoja alitoa maoni chanya, kuhusu mapinduzi makubwa yaliyofanywa katika Nyanja ya usafiri wa anga na kampuni hiyo ya ndege.
“Niliwahi kusafiri kwa ndege karibu miaka 17 iliyopita. Baada ya hapo sikuwahi kupanda ndege kabisa kwa maana niliona ni gharama kubwa ambazo sikuweza kuzimudu,” alisema Neyman Ndelijwa, 46, mkazi wa Arusha.
Neyman ambaye alikuwa kwenye ndege akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), akielekea Dar es Salaam, alimweleza mwandishi wa makala haya: “Sasa naweza kupanda ndege, Fast Jet wamerahisha sana maisha ya usafiri.
“Ukiangalia bei ambayo nimelipa, haitofautiani sana na gharama za kawaida za usafiri wa mabasi. Naamini kwamba hivi sasa kila anayesafiri kwa basi, anaweza kupanda ndege na ikawa nafuu zaidi kupitia Fast Jet.”
Anachokizungumza Neyman ni kweli kabisa, kwani mapinduzi ya sasa ya Fast Jet, yanafanya usafiri wa ndege kuwa gharama nafuu mno kupita hata basi.
Mathalan; kwa usafiri wa basi kwenda Mwanza, nauli ni kati ya shilingi 45,000 mpaka 60,000. Fast Jet yenyewe inatoza nauli ya chini kabisa shilingi 43,000, yaani usafiri shilingi 32,000 na kodi shilingi 11,000, jumla shilingi 43,000.
Vilevile unapopanda Fast Jet, haikulazimu kuingia gharama za ziada kwa ajili ya matumizi ya njiani. Kati ya dakika 45 na 60, unakuwa umeshafika unapokwenda.
Unaposafiri na basi, mbali na kutumia saa nyingi njiani, vilevile itakulazimu kununua chakula kuanzia asubuhi, mchana na wakati mwingine jioni, kwani unakuwa bado hujafika. Kwa kifupi, Fast Jet ni mkombozi wa kila Mtanzania.
Hakuna sababu ya kutumia saa nyingi njiani au wakati mwingine kupitisha zaidi ya siku ukisafiri, eti kwa kukimbia gharama za kusafiri kwa ndege, wakati Fast Jet inakusafirisha kwa bei nafuu kuliko hata ile ambayo ungelipa kwa basi.
Musika Nyangabo, 41, aliyekuwa anatokea JNIA kwenda Kia, alisema: “Fast Jet ni nafuu sana. Mimi na mtoto wangu tumeweza kusafiri kwenda na kurudi, Kilimanjaro – Dar kwa shilingi 282,000. Unadhani kama ingekuwa ni kwenye makampuni mengine hali ingekuwaje? Nafurahia bei na huduma za Fast Jet.”
NI HUDUMA KAMA ULAYA
“Ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, Watanzania wana kila sababu ya kujivunia Fast Jet kwa sababu ni kampuni bora sana ya ndege,” alisema Okite Obakponovwe, 37, raia wa Nigeria ambaye alizungumza na mwandishi wa makala haya, akiwa angani kutoka Kia kwenda Julius Nyerere International Airport, Dar es Salaam.
Mnigeria huyo, aliyekuwa Kilimanjaro kwa ajili ya kutalii Mlima Kilimanjaro, aliongeza: “Fast Jet ni sawa na Kampuni ya Easy Jet ya Uingereza. Kila huduma inayotolewa na Fast Jet, inaendana na Easy Jet, kwa kifupi Tanzania imepata bahati kuliko nchi nyingine yeyote Afrika.
Obakponovwe ambaye alikuwa ameongozana na mkewe, Irene Okite, aliongeza: “Gharama ni nafuu sana. Hata kule Uingereza Easy Jet ni nafuu. Mimi na mke wangu, tumefurahia huduma za Fast Jet, tumeweza kusafiri vizuri na ndege zake zina uhakika wa safari na kufika salama kwa asilimia 100.”
Abiria wengine waliozungumza na mwandishi wa makala haya ni Faraja Temu, aliyewasili Uwanja wa Ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume, Zanzibar akitokea Kilimanjaro, yeye alisema: “Nafurahia huduma, Fast Jet imerahisha maisha yetu ya usafiri hata kwetu sisi wanafunzi.”
NDEGE ZA AIRBUS BORA SANA
Mhudumu wa ndege, Jasmine Kaungu, alisema: “Nilishafanya kazi kwenye makampuni tofauti ya ndege hapa nchini, ila najisikia fahari kufanya kazi na Fast Jet. Abiria wanasafiri kwa uhakika sana kutokana na ndege zetu aina ya Airbus ambazo ni bora sana.”
Mmoja wa wasimamizi wa huduma kwa wateja, Omar Chinguile, alisema: “Kikubwa kwetu ni umakini. Menejimenti yetu ipo makini kuhakikisha wateja wanapata huduma bora sana. Ripoti yoyote inayoonesha uzembe, husababisha mfanyakazi apoteze ajira.”
BOOKING YA MAPEMA NI MUHIMU
Mkuu wa Oparesheni wa Fast Jet, Kia, Robert Kessy alisema: “Nashauri abiria wawe wanajitahidi kufanya booking mapema ili wapate bei ya chini kabisa ambayo ni shilingi 43,000. Wanapochelewa ndiyo hukutana na bei za juu. Kwa kawaida bei zetu zinaanzia shilingi 43,000 mpaka shilingi 300,000.”
GHANA YA TINGA FAINALI MWAKATUNDU CUP
Ghana Fc
TIMU ya soka ya Ghana Fc imeendelea kuonyesha ubabe katika mchezo wa soka baada ya kuichapa goli 1-0 timu ya Majengo Fc katika michuano ya Mwakatundu Cup katika uwanja wa shule ya msingi Mbata jijini hapa.Mchezo huo ulio kuwa umevuta hisia za mashabiki wengi katika jijini hapa kutokana na timu hizo kila zinzpokutana huwa kunakuwa na upinzani mkubwa kwani kila timu huwa inakamia kupata ushindi dhidi ya mwenzake.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kumfunga mwenzake kutokana kila timu kuwa makini na kutoruhusu wapinzani kushambulia ngome yao hali iliyo zua upinzani mkali katika mchezo huo.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ilkuweza kujipatia ushindi ambao utawezesha timu hiyo kutinga fainali,lakini timu ya Ghana ndiyo ilinufaika na mabadiliko hayo kwani ilijipatia goli la mapema katika kipindi chapili.
Baao la peke la Ghana Fc liliwekwa kimiani dakika ya 57 na Brayttoni Mponzi baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Majengo Fc nakuagiza shuti kali lililoenda kukwamisha mpira wavuni moja kwa moja.
Hadi dakika 90 za mchezo zina malizika Ghana ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli moja lililo wakatia tiketi ya kutinga fainari huku Mjengo wakiachwa na huzuni ya kuzimiwa ndoto yao ya kutinga fainali.
chanzo na Global
Airtel na Nokia wazindua Offer Kabambe ya Nokia Lumia 620
Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Batuli Chombo mwandishi wa habari wa Sikuba kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju
* Wateja kupata muda wa maongezi wa dakika 275 bure
* Offa itajumuisha SMS bila kikomo na kifurushi cha internet ya 3.75G cha 3GB
Monday 15 Aprili 2013, Airtel Tanzania imeungana kwa pamoja na kampuni ya Nokia na kuzindua simu ya Nokia Lumia 620 itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kuunganishwa na huduma ya technologia ya juu kwa
kupitia simu za kisasa na kupata ofa kabambe za bure za muda wa mongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet kwa muda wa mienzi mitatu Nokia Lumia 620 pamoja na simkadi ya Airtel itatoa uwezo tofauti ikiwemo kuunganishwa na internet na mtandao na kuangalia mitandao mbalimbali yakijamii pamoja na tovuti mbalimbali. Nokia Lumia inamuonekano mzuri na wa kisasa wenye rangi za kipekee ambapo kutokana na ubunifu `wetu wa kutengeneza simu zenye rangi tofauti mteja ataweza
kujichagulia simu yenye mvuto na rangi aitakayo
Vitu vingine vilivyopo kwenye simu hii ya Nokia Lumia ni pamoja na kamera yenye lensi ya kisasa, ya mega pixel 5, pamoja na kamera ya mbele, kutokana na kuwa na Lensi bora hii itamuwezesha mteja kupata video au picha yenye muonekano mzuri zaidi Ndani ya Nokia Lumia 620 unaweza kupata vitu muhimu sana ikiwemo ramani ya Dunia pamoja na maelekezo maalum wa vitu au sehemu maalum mbalimbali, Akiongea wakati wa uzinduzi Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema" tumeshirikiana na Nokia katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora na nafuu kwa kupitia vifaa vya Nokia vinavyokuhakikishia kiwango cha juu huku tukiwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu.
Kwa kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G tunayoitoa nchi nzima wateja wetu wana hakikishiwa huduma za uhakika wakati wote.Nokia Lumia itaunganishwa na ofa ya kifurushi cha muda wa maongezi cha dakika 275, sms bila kikomo na intenet ya kifurushi cha 3GB kitakachopatika kwa wiki moja kila mwenzi kwa muda wa mienzi mitatu "Kupata offa hii wateja wetu watatakiwa kuweka muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi 1000 mara wanaponunua simu ya Nokia Lumia 620. Na katika kuthibitisha thamira yetu ya kutoa huduma zinazoendana nathamani ya pesa ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu.
Airtel itaendelea kushirikiana na makampuni mbalimbali katika kutoa huduma bora na bei nafuu kwa kupitia mtandao wake mpana wenye huduma muhimu za Airtel Money na huduma yetu kabambe ya Airtel yatosha Aliongeza Mmbando.Kwa upande wake Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, alisema kampuni ya Nokia inaendelea kuonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kutoa bidhaa za simu bora zitakazowapatia wateja kile wanachokihitaji. Tunafurahia kuleta bidhaa bora na za bei nafuu zenye uwezo tofauti, simu ya Nokia Lumia 620katika soko la Tanzania,.Tunaamini muundo mzuri wa simu hii, rangi nzuri na uzoefu tofauti pamoja na huduma za Airtel zitawapatia wateja wetu sababu ya kujipatia simu hii ya Nokia Lumia"
"Nokia Lumia 620 zinapatikana kwa gharama ya shilingi 450,000/= tu.Simu inapatikana katika maduka yote ya Airtel, midcom na wakala wa Nokia wa premium. kwa sasa, kinachotakiwa kufanya ni wewe mtanzania kutembelea moja kati ya haya maduka na kujipatia simu hii orijino kutoka Nokia.Kutokana na ubora wa simu hizi za Nokia Lumia 620 mteja ataweza kufurahia zaidi huduma zote za kimtandao za Airtel zikiwemo zile za kutuma na kupokea pesa, Airtel Yatosha, Jirushe, kutuma na kupokea
SMS, huduma bora ya Intaneti ya 3.75G na nyingi nyinginezo.
Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa simu Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu
Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Jimy Tara mwandishi wa habari wa ITV kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju* Wateja kupata muda wa maongezi wa dakika 275 bure
* Offa itajumuisha SMS bila kikomo na kifurushi cha internet ya 3.75G cha 3GB
Monday 15 Aprili 2013, Airtel Tanzania imeungana kwa pamoja na kampuni ya Nokia na kuzindua simu ya Nokia Lumia 620 itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kuunganishwa na huduma ya technologia ya juu kwa
kupitia simu za kisasa na kupata ofa kabambe za bure za muda wa mongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet kwa muda wa mienzi mitatu Nokia Lumia 620 pamoja na simkadi ya Airtel itatoa uwezo tofauti ikiwemo kuunganishwa na internet na mtandao na kuangalia mitandao mbalimbali yakijamii pamoja na tovuti mbalimbali. Nokia Lumia inamuonekano mzuri na wa kisasa wenye rangi za kipekee ambapo kutokana na ubunifu `wetu wa kutengeneza simu zenye rangi tofauti mteja ataweza
kujichagulia simu yenye mvuto na rangi aitakayo
Vitu vingine vilivyopo kwenye simu hii ya Nokia Lumia ni pamoja na kamera yenye lensi ya kisasa, ya mega pixel 5, pamoja na kamera ya mbele, kutokana na kuwa na Lensi bora hii itamuwezesha mteja kupata video au picha yenye muonekano mzuri zaidi Ndani ya Nokia Lumia 620 unaweza kupata vitu muhimu sana ikiwemo ramani ya Dunia pamoja na maelekezo maalum wa vitu au sehemu maalum mbalimbali, Akiongea wakati wa uzinduzi Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema" tumeshirikiana na Nokia katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora na nafuu kwa kupitia vifaa vya Nokia vinavyokuhakikishia kiwango cha juu huku tukiwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu.
Kwa kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G tunayoitoa nchi nzima wateja wetu wana hakikishiwa huduma za uhakika wakati wote.Nokia Lumia itaunganishwa na ofa ya kifurushi cha muda wa maongezi cha dakika 275, sms bila kikomo na intenet ya kifurushi cha 3GB kitakachopatika kwa wiki moja kila mwenzi kwa muda wa mienzi mitatu "Kupata offa hii wateja wetu watatakiwa kuweka muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi 1000 mara wanaponunua simu ya Nokia Lumia 620. Na katika kuthibitisha thamira yetu ya kutoa huduma zinazoendana nathamani ya pesa ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu.
Airtel itaendelea kushirikiana na makampuni mbalimbali katika kutoa huduma bora na bei nafuu kwa kupitia mtandao wake mpana wenye huduma muhimu za Airtel Money na huduma yetu kabambe ya Airtel yatosha Aliongeza Mmbando.Kwa upande wake Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, alisema kampuni ya Nokia inaendelea kuonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kutoa bidhaa za simu bora zitakazowapatia wateja kile wanachokihitaji. Tunafurahia kuleta bidhaa bora na za bei nafuu zenye uwezo tofauti, simu ya Nokia Lumia 620katika soko la Tanzania,.Tunaamini muundo mzuri wa simu hii, rangi nzuri na uzoefu tofauti pamoja na huduma za Airtel zitawapatia wateja wetu sababu ya kujipatia simu hii ya Nokia Lumia"
"Nokia Lumia 620 zinapatikana kwa gharama ya shilingi 450,000/= tu.Simu inapatikana katika maduka yote ya Airtel, midcom na wakala wa Nokia wa premium. kwa sasa, kinachotakiwa kufanya ni wewe mtanzania kutembelea moja kati ya haya maduka na kujipatia simu hii orijino kutoka Nokia.Kutokana na ubora wa simu hizi za Nokia Lumia 620 mteja ataweza kufurahia zaidi huduma zote za kimtandao za Airtel zikiwemo zile za kutuma na kupokea pesa, Airtel Yatosha, Jirushe, kutuma na kupokea
SMS, huduma bora ya Intaneti ya 3.75G na nyingi nyinginezo.
MUME AMWAGIA MAJI YA MOTO MKEWE
Janet Udegba
Nini tafsiri ya uelekeo wa dunia kutokana na matukio ya kutisha? Upo ukatili mkubwa umefanyika nchini Nigeria ambapo mume amemwagia mkewe mafuta ya petroli na kumchoma moto.Kehinde Adesamuye, 39, mkazi wa Lagos, Nigeria anadaiwa kumchoma kwa moto wa petroli hivi karibuni mkewe Janet Udegba, 35, katika Mtaa wa Ikotun jijini Lagos baada ya kuwa na hasira kutokana na kuhisi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine.
Janet na Mumewe Kehinde Adesamuye
Janet alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa katika eneo lake la biashara akiuza vyakula kabla ya Kehinde kufika hapo usiku huo na kumwagia petroli mgongoni kisha kuwasha moto kwa kutumia kibiriti.Hata hivyo, alisema Wanigeria hawatamwachia huru Kehinde kutokana na kile alichokifanya. Akisimulia mgogoro wao, anasema:
Mume wangu amekuwa na wivu daima. Amekuwa na tabia ya kunipiga kila wakati. Nimejaribu mara nyingi kuachana naye lakini huwa ananitishia kuwa lazima atanidhuru. Niliendelea kuishi naye kwa kuwa nilikuwa na hofu ya maisha yangu, aliwahi kuniambia kuwa sitaweza kutoroka hata siku moja“Serikali lazima ihakikishe kuwa Kehinde analipa kwa kile alichonifanyia. Mimi ni yatima, ninafanya biashara ya vyakula ili niishi. Sasa nimetumia pesa zangu zote kwa ajili ya matibabu. Kwa kweli kwa sasa nahitaji msaada,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.
Kehinde alijaribu kutuma rafiki zake ili wamwombee msamaha kwa Janet lakini alikataa. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.
chanzo na global.
Subscribe to:
Posts (Atom)